UGANDA YAOMBA KUTUMIA UWANJA WA MKAPA MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2022.

UGANDA YAOMBA KUTUMIA UWANJA WA MKAPA MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2022.

Timu ya Taifa ya Uganda inatarajiwa kutumia Uwanja wa Taifa wa Tanzania kama uwanja wao wa nyumbani kwenye michuano ya kufuzu Kombe la Dunia la 2022. Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) limelijulisha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya msaada wanaohitaji wa kutumia Uwanja wa Mkapa kama uwanja wao wa nyumbani ikiwa watashindwa kupata Uwanja

Timu ya Taifa ya Uganda inatarajiwa kutumia Uwanja wa Taifa wa Tanzania kama uwanja wao wa nyumbani kwenye michuano ya kufuzu Kombe la Dunia la 2022.

Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) limelijulisha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya msaada wanaohitaji wa kutumia Uwanja wa Mkapa kama uwanja wao wa nyumbani ikiwa watashindwa kupata Uwanja unaokidhi Vigezo.

FUFA bado haijafikia maamuzi juu ya Uwanja wa St Mary’s Kitende ambao ulikuwa ukitumika hivi karibuni kwenye michuano ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwakuwa barabara kuelekea kwenye uwanja huo zinapitika kwa shida.

Hivi sasa FUFA inaendelea kusubiri maamuzi ya uchunguzi wa mwisho uliofanya katika uwanja huo huku jitihada za kutafuta mbadala zikiendelea.

Uwanja wa Nelson Mandela ambao ni Uwanja wa Taifa wa Uganda, ulitangazwa kutostahili kuandaa mechi za kimataifa baada ya ukaguzi na CAF na FIFA mnamo mwezi Machi 2020.

Hali mbaya ya uwanja wa kuchezea na vyumba vya kubadilishia nguo ilikuwa kati ya vitu vilivyoonekana kuwa chini ya viwango.

Kwenye haya Mashindano ya kufuzu kombe la Duni 2022, Uganda ipo Kundi E pamoja na Kenya, Rwanda na Mali.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »